Swali: Ni lipi kosa la Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Imepokelewa katika upokezi mwingine ya kwamba ni pale alipomwomba Mola wake kumuokoa mtoto wake:

وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ قَالَ يَا نُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ ۖ إِنَّهُ عَمَلٌ غَيْرُ صَالِحٍ ۖ فَلَا تَسْأَلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۖ إِنِّي أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ

”Nuuh akamwita Mola wake, akasema: ”Mola wangu! Hakika mwanangu ni katika ahli zangu na hakika ahadi Yako ni ya kweli Nawe ni mwadilifu zaidi wa kuhukumu kuliko mahakimu wote.” Akasema: ”Ee Nuuh! Hakika huyo si katika ahli zako, hakika yeye matendo yake si mema. Hivyo basi usiniombe yale usiyokuwa na elimu nayo, Mimi nakusihi usijekuwa katika wajinga.”[1]

[1] 11:45-46

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24377/ما-خطيىة-نوح-عليه-السلام
  • Imechapishwa: 04/10/2024