Ahmad bin Salamah amesema:

“Muslim alikuwa na kikao kwa ajili ya kujikumbusha. Akasikia Hadiyth ambayo hajawahi kuisikia, akaenda nyumbani kwake, akawasha mataa na akawaambia watu wa nyumbani: “Asiingie yeyote katika nyinyi.” Akaambiwa: “Tumeletewa kikapu cha tende.” Akasema: “Kileteni.” Wakamletea nacho na akaanza kuitafuta Hadiyth na huku anakula tende moja baada ya nyingine. Kulipoingia asubuhi  tende zikaisha na akaipata Hadiyth.”

Ameipokea Abu ´Abdillaah al-Haakim ambaye amesema:

“Kuna rafiki mwaminifu aliyenambia kwamba ndio ilikuwa sababu ya kufa kwake.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/564)
  • Imechapishwa: 26/11/2020