Kipi bora ndani ya Ramadhaan kwa aliyeko Makkah?

Swali: Ni kipi bora ndani ya Ramadhaan kwa muislamu; kusoma Qur-aan, kufanya Twawaaf au kuswali swalah zinazopendeza?

Jibu: Afanye kile kitachokuwa chepesi katika haya; mara asome Qur-aan, wakati mwingine atufu na wakati mwingine aswali. Kwa maana nyingine kila atachokiweza katika haya katika swalah, Twawaaf, kisomo, kuomba du´aa, Tasbiyh na Tahliyl. Awe ni mwenye kujitahidi yote haya. Mara hiki mara kile. Aharakie kufanya kila aina ya kheri; mara atufu, mara aswali, mara asome.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 23/04/2023