Swali: Nilikwenda Hajj pamoja na baba yangu na tukapata fedha kiasi cha 2,250 SAR za kisaudia katika eneo la ”Jamrat-ul-Wustwaa”. Baba yangu akazitoa fedha hizo kama swadaqah kwa msikiti wake. Ni ipi hukumu ya jambo hilo?
Jibu: Inapasa kwa yeyote atakayekuta kitu kilichopotea katika Makkah au Madiynah asitoe sadaka msikitini wala sehemu nyingine. Bali anatakiwa kuitangaza mara kwa mara ndani ya Haram kwa kusema: Ni nani mwenye fedha? Ni nani mwenye dhahabu? Ni nani mwenye kitu hiki? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kilichopotea katika Haram hakihalaliki kwa yeyote isipokuwa kwa yule atakayekitangaza.”
Hivyo hairuhusiwi kukitoa kwa msikiti wala kwa kitu kingine chochote. Bali hutangazwa mpaka mwenyewe aje kukichukua. Ikiwa mtu hawezi kukitangaza kila mara huko Makkah, basi kuna idara maalum iliyowekwa kwa ajili ya kupokea vitu vilivyopotea. Akivikabidhi huko basi atakuwa ametekeleza wajibu wake hadi mwenyewe atakapokuja kuulizia. Ama kuzipa masikini, kuzitumia kwenye kilimo au kuzitoa kwa msikit, hilo halifai. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hazihalaliki zilizopotea katika Haram isipokuwa kwa anayezitangaza.”
Imekuja katika riwaya nyingine:
“Ispokuwa kwa mwenye kukitangaza kwa kusema: ni nani mwenye dhahabu? Ni nani mwenye…?”
Vivyo hivyo hukumu hii ipo kwa Madiynah pia.
Swali: Vipi akiziacha bila kuzichukua?
Jibu: Akiziacha, basi hakuna tatizo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1067/حكم-لقطة-مكة
- Imechapishwa: 27/01/2026
Swali: Nilikwenda Hajj pamoja na baba yangu na tukapata fedha kiasi cha 2,250 SAR za kisaudia katika eneo la ”Jamrat-ul-Wustwaa”. Baba yangu akazitoa fedha hizo kama swadaqah kwa msikiti wake. Ni ipi hukumu ya jambo hilo?
Jibu: Inapasa kwa yeyote atakayekuta kitu kilichopotea katika Makkah au Madiynah asitoe sadaka msikitini wala sehemu nyingine. Bali anatakiwa kuitangaza mara kwa mara ndani ya Haram kwa kusema: Ni nani mwenye fedha? Ni nani mwenye dhahabu? Ni nani mwenye kitu hiki? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kilichopotea katika Haram hakihalaliki kwa yeyote isipokuwa kwa yule atakayekitangaza.”
Hivyo hairuhusiwi kukitoa kwa msikiti wala kwa kitu kingine chochote. Bali hutangazwa mpaka mwenyewe aje kukichukua. Ikiwa mtu hawezi kukitangaza kila mara huko Makkah, basi kuna idara maalum iliyowekwa kwa ajili ya kupokea vitu vilivyopotea. Akivikabidhi huko basi atakuwa ametekeleza wajibu wake hadi mwenyewe atakapokuja kuulizia. Ama kuzipa masikini, kuzitumia kwenye kilimo au kuzitoa kwa msikit, hilo halifai. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hazihalaliki zilizopotea katika Haram isipokuwa kwa anayezitangaza.”
Imekuja katika riwaya nyingine:
“Ispokuwa kwa mwenye kukitangaza kwa kusema: ni nani mwenye dhahabu? Ni nani mwenye…?”
Vivyo hivyo hukumu hii ipo kwa Madiynah pia.
Swali: Vipi akiziacha bila kuzichukua?
Jibu: Akiziacha, basi hakuna tatizo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1067/حكم-لقطة-مكة
Imechapishwa: 27/01/2026
https://firqatunnajia.com/kiokotwa-cha-makkah-na-madiynah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket