Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa kila Shiy´iy ni Raafidhwiy au kinyume chake?
Jibu: Hapana. Shiy´ah ni neno lililoenea ambalo linakusanya mapote yao yote. Wale walioandika kuhusu mapote wanasema kuwa Shiy´ah wamegawanyika karibu makundi ishirini na mbili. Katika wao wako ambao ni makafiri na wengine wazushi kutegemea yale wanayoamini. Yako mapote sita ya Zaydiyyah ambao ni wazushi.
Kuhusu Raafidhwah wao ni wapetukaji. Wameitwa Raafidhwah kwa sababu walimkataa Zayd bin ´Aliy wakati walipomuuliza kuhusu Abu Bakr na ´Umar ambapo akawajibu kwamba wao ni mawaziri wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakakataa hayo ambapo akawaambia: “Mmenikataa. Nendeni zenu nyinyi ni Raafidhwah (wakataaji)”. Kabla ya hapo walikuwa wakiitwa Khashbiyyah. Kwa sababu hawapigani isipokuwa kwa mbao. Hawapigani kwa panga. Tangu hapo ndipo wakaitwa Raafidhwah. Wao ndio wale ambao wanawakufurisha Maswahabah na kuwatukana. Vilevile wanawaabudu watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayh iwa sallam) na kutawasali kwao.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
- Imechapishwa: 07/08/2018
Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa kila Shiy´iy ni Raafidhwiy au kinyume chake?
Jibu: Hapana. Shiy´ah ni neno lililoenea ambalo linakusanya mapote yao yote. Wale walioandika kuhusu mapote wanasema kuwa Shiy´ah wamegawanyika karibu makundi ishirini na mbili. Katika wao wako ambao ni makafiri na wengine wazushi kutegemea yale wanayoamini. Yako mapote sita ya Zaydiyyah ambao ni wazushi.
Kuhusu Raafidhwah wao ni wapetukaji. Wameitwa Raafidhwah kwa sababu walimkataa Zayd bin ´Aliy wakati walipomuuliza kuhusu Abu Bakr na ´Umar ambapo akawajibu kwamba wao ni mawaziri wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakakataa hayo ambapo akawaambia: “Mmenikataa. Nendeni zenu nyinyi ni Raafidhwah (wakataaji)”. Kabla ya hapo walikuwa wakiitwa Khashbiyyah. Kwa sababu hawapigani isipokuwa kwa mbao. Hawapigani kwa panga. Tangu hapo ndipo wakaitwa Raafidhwah. Wao ndio wale ambao wanawakufurisha Maswahabah na kuwatukana. Vilevile wanawaabudu watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayh iwa sallam) na kutawasali kwao.
Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
Imechapishwa: 07/08/2018
https://firqatunnajia.com/kila-shiyiy-ni-raafidhwiy-au-kinyume-chake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)