Swali: Mimi ni kijana ninaishi na baba na mama yangu na bado sijaoa. Je, Zakaat-ul-Fitwr yangu natolewa na baba yangu au natoa kwa mali yangu binafsi?
Jibu: Zakaat-ul-Fitwr ni wajibu na faradhi. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefaradhisha Zakaat-ul-Fitwr pishi[1] ya tende au pishi ya shayiri kwa mdogo na mkubwa, muungwana na mtumwa, mvulana na msichana katika waislamu.”
Ni kama mambo mengine ya wajibu ambayo anazungumzishwa kila mmoja kivyake. Wewe ndiye mwenye kusemezwa na hivyo unatakiwa kujitolea zakaah kivyako hata kama uko na baba na kaka. Vilevile mke ni mwenye kuzungumzishwa na hivyo anatakiwa kujitolea zakaah kivyake hata kama yuko na mume.
Lakini mkuu wa familia akitaka kuitolea familia yake zakaah hakuna neno kufanya hivo. Ikiwa mtu huyu yuko na baba ambaye anamuhudumia na akapenda kumtolea zakaah mwanae hakuna neno kufanya hivo.
[1] Ibn Baaz (Rahimahullaah) amesema: ”Pishi moja ni sawa na takriban 3 kg.” (Majmuu´-ul-Fataawaa (14/201))
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/261)
- Imechapishwa: 21/06/2017
Swali: Mimi ni kijana ninaishi na baba na mama yangu na bado sijaoa. Je, Zakaat-ul-Fitwr yangu natolewa na baba yangu au natoa kwa mali yangu binafsi?
Jibu: Zakaat-ul-Fitwr ni wajibu na faradhi. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefaradhisha Zakaat-ul-Fitwr pishi[1] ya tende au pishi ya shayiri kwa mdogo na mkubwa, muungwana na mtumwa, mvulana na msichana katika waislamu.”
Ni kama mambo mengine ya wajibu ambayo anazungumzishwa kila mmoja kivyake. Wewe ndiye mwenye kusemezwa na hivyo unatakiwa kujitolea zakaah kivyako hata kama uko na baba na kaka. Vilevile mke ni mwenye kuzungumzishwa na hivyo anatakiwa kujitolea zakaah kivyake hata kama yuko na mume.
Lakini mkuu wa familia akitaka kuitolea familia yake zakaah hakuna neno kufanya hivo. Ikiwa mtu huyu yuko na baba ambaye anamuhudumia na akapenda kumtolea zakaah mwanae hakuna neno kufanya hivo.
[1] Ibn Baaz (Rahimahullaah) amesema: ”Pishi moja ni sawa na takriban 3 kg.” (Majmuu´-ul-Fataawaa (14/201))
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/261)
Imechapishwa: 21/06/2017
https://firqatunnajia.com/kila-mmoja-atakiwa-kujitolea-zakaat-ul-fitwr-yake/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket