Baba aliyesafiri anamuwakilisha mwanawe kutoa Zakaat-ul-Fitwr

Swali: Kuna mtu ni mfanya kazi ambaye anafanya kazi nje ya nchi yake mbali na wao. Mwisho wa Ramadhaan alipotaka kwenda kazini kwake akamuwakilisha mtoto wake ili yeye ndiye amtolee Zakaat-ul-Fitwr na awatolee vilevile wengine. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi?

Jibu: Hakuna neno. Inafaa kwa mtu kuwawakilisha watoto wake wamtolee Zakaat-ul-Fitwr katika wakati wake kwa sababu ya yeye kwenda katika mji mwingine kwa ajili ya kazi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/262)
  • Imechapishwa: 21/06/2017