Swali: Mimi nina bibi ambaye miaka yake sasa imepita mia moja na arubaini na bado anaishi na anaweza kutembea masafa mafupi. Lakini hajui baadhi ya mambo ya wajibu ya swalah. Kila ambavyo najaribu kumfunza Tashahhud, al-Faatihah na baadhi ya Suurah zengine za Qur-aan fupi na anayotakiwa kusema katika swalah yake basi hawezi anashindwa kufahamu vizuri na anasahau baada ya siku mbili yale niliyomwambia. Je, napata dhambi kwa ajili yake kwa sababu mimi ndiye namfunza?

Jibu: Hupati dhambi kwa ajili yake ukisimama na wajibu wa kumfunza. Ukimfunza na anasahau basi hupati dhambi. Lakini rudi kumfunza mara kwa mara. Ni mama yako au bibi yako na hivyo unatakiwa kumfanyia pupa ya kupitiliza na khaswa ukizingatia kwamba amefikia umri wa ukongwe. Anahitajia kufuatiliwa na kufunzwa ili asisahau. Yale yaliyo nje ya uwezo wako, basi ni kwamba Allaah hakukalifishi kwayo. Amesema (Ta´ala) amesema:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kiasi cha inavyoweza.”   (2:286)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (02) http://binothaimeen.net/content/6637
  • Imechapishwa: 16/03/2019