Kijana anataka kuoa msichana fulani na mzazi ataka mwingine

Swali: Nimtii baba yangu kama nataka kuoa katika familia fulani na baba yangu anataka nioe katika familia nyingine na nikifanya hivyo ni katika wema?

Jibu: Ndio, kiwa mwanamke anayemtaka baba yako ni mwanamke mzuri na mwema, mtii baba yako katika hilo. Ni katika kumfanyia wema. Ikiwa mwanamke sio mwema, usimtii mzazi wako katika jambo hili ambalo si la sawa kwako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (61) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-03-11.MP3
  • Imechapishwa: 21/08/2020