Swali: Baadhi ya wauzaji hawauzi kitu mpaka waape kwacho.

Jibu: Haitakikani, kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokataza hayo. Haitakikani kuapa wakati wa biashara. Hadiyth inasema:

”Watu aina tatu Allaah hatowazungumzisha… ” ambapo mmoja wapo akasema ”… mtu ambaye amemfanya Allaah kuwa ndio bidhaa Yake; ambapo hauzi isipokuwa kwa kiapo chake na wala hanunui isipokuwa kwa kiapo chake.”

Kwa hivyo inatakiwa kuchunga kiapo. Allaah anasema:

وَلَا تَجْعَلُوا اللَّـهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَانِكُمْ

“Wala msimfanye Allaah kuwa ni nyudhuru ya viapo vyenu.” (02:224)

Hata hivyo hapana vibaya ikiwa kiapo ni kwa ajili ya kutilia mkazo kheri, kulingania kheri na kutahadharisha shari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23956/حكم-الحلف-على-البيع-والشراء
  • Imechapishwa: 03/08/2024