Swali: Je, bado analazimika kutoa kafara akiapa kabla ya kubaleghe na akajirejea baada ya kubaleghe?

Jibu: Wanazuoni wametofautiana juu ya viapo vya watoto kama vinafungika au havifungiki kabla ya wao kubaleghe. Udhahiri ni kwamba havifungiki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu watatu; aliyelala hadi aamke, mdogo hadi awe mkubwa na mwendawazimu hadi apate fahamu.”[1]

[1] Abu Daawuud (4405) na Ahmad (1362). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2/5).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24018/هل-تنعقد-ايمان-الصغار-وتلزمهم-كفارة
  • Imechapishwa: 17/08/2024