Swali: Nini manaa ya kuieleza Khutbah yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa ni yenye balagha?

Jibu: Inamaanisha kuwa ilikuwa Khutbah tukufu sana, alifafanua ndani yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ukamilifu, akamsifu Allaah, akamtukuza, akawakumbusha watu na akazidisha kuwaonya ili waogope adhabu ya Allaah. Khutbah yenye balagha ni ile iliyo na mawaidha, ukumbusho na maonyo kwa maneno wazi na yenye kueleweka, pamoja na ukali na kuonyesha khofu juu ya watu na tahadhari kwao. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikhutubu kwa hasira kali, sauti yake ikipanda, macho yake yakigeuka mekundu kana kwamba anawaonya jeshi, akisema:

“Limekujieni asubuhi au jioni.”

Si Khutbah dhaifu isiyo na uhai. Wapo baadhi ya watu wanapokhutubu maneno yao ni dhaifu na hayana uhai. Hayatikisi nyoyo. Tofauti na yule anayekhutubu kwa nguvu na balagha, akitumia maneno yenye athari, sauti yenye kutikisa, pamoja na kuchagua maneno yanayoingia moyoni na kuonyesha huzuni na khofu kwa wale wanaowakhutubia.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31496/معنى-وصف-خطبة-النبي-عليه-الصلاة-والسلام-بانها-بليغة
  • Imechapishwa: 29/10/2025