Swali: Je, imesuniwa katika Khutbah ya kupatwa jua au mwezi kusimama?

Jibu: Katika baadhi ya mapokezi imesemekana kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipanda mimbari akawakhutubia. Ni jambo lenye wasaa; akipanda mimbari au akasimama au akawakhutubia akiwa amekaa, yote ni sahihi. Lililo muhimu ni kuwakumbusha watu.

Swali: Vipi akikhutubu hali ya kukaa?

Jibu: Dhahiri ni kwamba lengo litakuwa limefikiwa, khaswa ikiwa idadi yao ni ndogo na hakuna haja ya kutumia mimbari. Lakini ikiwa kuna haja ya mimbari au kuna kipaza sauti, basi inatosha. Makusudio yamefikiwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31497/هل-يشرع-الوقوف-في-خطبة-الكسوف
  • Imechapishwa: 25/10/2025