Swali: Nimesoma katika ufafanuzi wa Ibn Battwaal wa ”as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy ya kwamba wanachuoni wameafikiana juu ya kwamba Khawaarij ni katika jumla ya waumini. Je, Khawaarij ni makafiri au hapana?
Jibu: Maafikiano sio sahihi. Kuna ambao wanawakufurisha Khawaarij. Mimi mwenyewe siwakufurishi makafiri isipokuwa wale waliokufuru. Khawaarij wamegawanyika katika mapote mengi. Miongoni mwao kuna makafiri. Kama ambavyo Raafidhwah wamegawanyika mapote mengi. Kuna ambao ni makafiri, kama walivyo Khawaarij. Kuna wengine bado ni waislamu na wanaingia katika Ahl-ul-Bid´ah na mapote potevu aliyoelezea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mayahudi wamefarikiana katika mapote sabini na moja. Manaswara wamefarikiana katika mapote sabini na mbili. Na Ummah wangu utafarikiana katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni wepi, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni lile litakalofuata yale ninayofuata mimi hii leo na Maswahabah wangu.”[1]
Katika upokezi mwingine imekuja:
“Mkusanyiko.”[2]
Wao ni katika mapote potevu na ni katika mapote mabaya kabisa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yao:
“Wao ni viumbe na walimwengu waovu kabisa.”[3]
Ameamrisha kuwaua. Pamoja na hivyo ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) hakuwakufurisha. Hata hivyo kuna wanachuoni wanaowakufurisha. Mmoja wao ni Ahmad katika moja ya maoni yake.
[1] Abu Daawuud (4596) na at-Tirmidhiy (264) kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “al-Mishkaah” (171).
[2] Ahmad (03/145), Abu Daawuud (4597), Ibn Maajah (4040) na al-Haakim (01/128).[2]
[3] Muslim (1067) na Ahmad (05/31).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kashf-us-Sitaar, uk. 10-12
- Imechapishwa: 29/10/2016

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kashf-us-Sitaar, uk. 10-12
Imechapishwa: 29/10/2016
https://firqatunnajia.com/khawaarij-ni-makafiri/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)