Khatwiyb anayeswali na kusoma Qur-aan nyumbani ana thawabu za aliyejitolea ngamia siku ya ijumaa?

Swali: Khatwiyb akiswali Sunnah nyumbani kwake na akasoma Qur-aan anakuwa kama ambaye amekurubisha ngamia[1] akianza kufanya hivo ule mwanzoni mwa wakati?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kunatarajiwa kwake kheri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa anakuja isipokuwa wakati wa Khutbah. Kunatarajiwa kwake kheri – Allaah akitaka – ikiwa ameizuia nafsi yake kwa sababu ya kufuata Sunnah.

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (708).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23805/كيف-يكون-فضل-التبكير-لخطيب-الجمعة
  • Imechapishwa: 03/05/2024