Swali: Mwanaume anafanya kazi ya kuwachukua picha wanaume na wanawake.
Jibu: Ni maovu. Ni chumo baya.
Swali: Je, inafaa kula kichinjwa chake?
Jibu: Haifai ikiwa kinatokana na chumo hili. Lakini ni sawa kula katika chumo lake ikiwa yuko na mapato mengine.
Swali: Akiwa na mapato mengine?
Jibu: Ni sawa. Ni kama mayahudi wako na machumo mengi na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akala machumo yake.
Swali: Hukumu ya kutangamana naye.
Jibu: Anatakiwa kunasihiwa na kuongozwa katika kheri kama watenda maasi wengine. Asifanywe ni mtu wa kutangamana naye na rafiki. Mnasihi kuwa ni mja wa Allaah, kwamba anachokifanya hakifai na amche Allaah. Mweleze kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22669/حكم-من-يعمل-في-تصوير-النساء-والرجال
- Imechapishwa: 13/07/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)