Katika hali hii msafiri anapaswa kukamilisha

Swali: Msafiri akiswali nyuma ya mwenyeji?

Jibu: Msafiri anatakiwa kuswali Rak´ah nne kamili anaposwali nyuma ya mwenyeji kama maamuma. Hii ndio Sunnah, kama ilivyosimuliwa katika Hadiyth iliyopokelewa na Muslim kutoka kwa Ibn ´Abbaas:

“Sunnah ni kwamba msafiri akiswali nyuma ya mwenyeji, aswali nne.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24908/هل-يتم-المسافر-الصلاة-اذا-اىتم-بالمقيم
  • Imechapishwa: 03/01/2025