Katika hali hii kazi ya uanasheria haitofaa

Swali: Vipi kazi ya uanasheria?

Jibu: Haina neno endapo atamcha Allaah. Ni kama kazi ya uwakala; mtu akimcha Allaah na akachunga ukweli haina neno ni kama mfano wa uwakala. Ni kama mfano wa yule unayemuwakilisha akutetee.

Swali: Ijapo itakuwa ni kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na watu?

Jibu: Hapana, haijuzu kwa sheria zilizotungwa na watu. Haijuzu. Uanasheria kwa mujibu wa Shari´ah.

Swali: Kunafunzwa sheria zilizotungwa na watu?

Jibu: Ninachokusudia ni kwamba haitofaa ikiwa anatetea kwa kutumia hukumu isiyokuwa Shari´ah ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23224/حكم-العمل-في-مهنة-المحاماة
  • Imechapishwa: 29/11/2023