Swali: Je, inafaa kukata swalah ya mamkuzi ya msikiti kunapokimiwa swalah katika ile Rak´ah ya kwanza?
Jibu: Imepokelewa katika Hadiyth ya kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kunapokimiwa swalah basi hakuna swalah nyingine isipokuwa ile ya faradhi.”[1]
Wanazuoni wamesema kuwa hiyo inafasiriwa ikiwa ni pale mwanzoni. Kwa msemo mwingine ameanza swalah na papohapo kukakimiwa swalah. Lakini kukikimiwa swalah baada ya kuinua kichwa chake kutoka katika Rukuu´ katika ile Rak´ah ya pili ya swalah iliyopendekezwa, basi anatakiwa kuikamilisha. Kwa sababu sehemu iliyobaki sio swalah kamili na hivyo hakuna neno.
[1] Muslim (710).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/هل-يجوز-قطع-تحية-المسجد-إذا-أقيمت-الصلاة؟
- Imechapishwa: 18/06/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)