Swalii: Kuna mtu anataka kuchinja Udhhiyah na yuko na deni. Hivyo anataka kuchukua mkopo ili anunue mnyama wa Udhhiyah.

Jibu: Mimi naona kuwa asifanye hivo isipokuwa akiwa ni mtu ambaye ana uhakika kuwa atalipa deni hilo. Mtu huyu tunasema kuwa amehuisha Sunnah na amefanya kheri. Midhali kwa mfano anajua kuwa hivi sasa hana kitu lakini huko baadaye atapopata mshahara wake atakuwa na kitu, hakuna neno akachukua mkopo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (73) http://binothaimeen.net/content/1685
  • Imechapishwa: 11/08/2019