Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Hapana swalah wakati chakula kishatengwa wala wakati mtu anazuia haja kubwa na ndogo.”
Je, maoni yenye nguvu zaidi kuhusu ukanushaji huu ni kwamba ni ukanushaji wa kusihi au ukanushaji wa ukamilifu?
Jibu: Wanazuoni wengi wanaona kuwa ni ukanushaji wa kusihi na kwamba akiswali swalah yake ni sahihi, ingawa inachukiza. Maoni yanayosema kuwa ukanushaji ni wa kusihi kwa swalah ni yenye nguvu. Lakini ikiwa kuzuia huko ni kukubwa, basi haimpasi mtu kuswali. Vivyo hivyo ikiwa nafsi yake inakitamani sana chakula. Lakini ikiwa kuzuia huko si kukubwa na akaswali, basi ninatarajia kwamba swalah yake ni sahihi. Kwa hali yoyote lililo bora kwake ni kujisaidia kwanza, kisha aswali ili aielekee swalah yake vizuri na ili asiwe mwenye kushughulishwa na jambo hilo. Vivyo hivyo ikiwa anahitaji chakula na chakula kimewekwa mbele yake, basi aanze kula chakula.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
- Imechapishwa: 19/09/2026
Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Hapana swalah wakati chakula kishatengwa wala wakati mtu anazuia haja kubwa na ndogo.”
Je, maoni yenye nguvu zaidi kuhusu ukanushaji huu ni kwamba ni ukanushaji wa kusihi au ukanushaji wa ukamilifu?
Jibu: Wanazuoni wengi wanaona kuwa ni ukanushaji wa kusihi na kwamba akiswali swalah yake ni sahihi, ingawa inachukiza. Maoni yanayosema kuwa ukanushaji ni wa kusihi kwa swalah ni yenye nguvu. Lakini ikiwa kuzuia huko ni kukubwa, basi haimpasi mtu kuswali. Vivyo hivyo ikiwa nafsi yake inakitamani sana chakula. Lakini ikiwa kuzuia huko si kukubwa na akaswali, basi ninatarajia kwamba swalah yake ni sahihi. Kwa hali yoyote lililo bora kwake ni kujisaidia kwanza, kisha aswali ili aielekee swalah yake vizuri na ili asiwe mwenye kushughulishwa na jambo hilo. Vivyo hivyo ikiwa anahitaji chakula na chakula kimewekwa mbele yake, basi aanze kula chakula.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
Imechapishwa: 19/09/2026
https://firqatunnajia.com/katika-hali-hii-anza-kula-na-kujisaidia-kwanza/