al-Hajuuriy ametahadharisha baadhi ya ndugu na akalitahadharisha vilevile genge lake na wafuasi wake kutokamana na watu hao na kundi kubwa la wanafunzi waheshimiwa ambao Salafiyyah yao inatambulika na hakwenda kinyume naye. Amefutu juu ya kuwakata na wakawa ni wenye kusema:
“Tumesikia na tumetii.”
Isitoshe ametahadharisha chuo kikuu cha Kiislamu [cha al-Madiynah][1] na wakahadhari pamoja naye. Walitofautiana na Shaykh ´Ubayd kuhusu mada hiyo lakini hata hivyo wakasimama upande wa al-Hajuuriy. al-Hajuuriy vilevile akatofautiana na [Muhammad] al-Wasswaabiy lakini hata hivyo wakasimama upande wa al-Hajuuriy dhidi ya mwalimu wake. Akatofautiana vilevile na Shaykh Muhammad bin Haadiy [al-Madkhaliy] lakini hata hivyo wakasimama upande wa al-Hajuuriy na wakamtukana Shaykh Muhammad. al-Hajuuriy akatofautiana na Shaykh ´Abdullaah al-Bukhaariy nao wakatofautiana na al-Bukhaariy kwa kumfuata Shaykh wao. Sivyo tu aliwatuhumu wanachuoni kuwa wanaifanyia njama Daar-ul-Hadiyth iliyoko Dammaaj na wakawa ni wenye kumfuata. Vilevile akawatuhumu ya kwamba wanajifanya wao kuwa ndio viongozi wa Da´wah Salafiyyah ambapo wakamsadikisha. Amefutu kwa fataawaa nyingi za kimakosa wakachukulia sahali na wakamtetea kwa nguvu zao zote. Kulitolewa mashairi yenye kuvuka mipaka kuhusu al-Hajuuriy[2] wakanyamaza na hawakuzungumza. al-Hajuuriy amemvulia adabu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[3] hata hivyo wakanyamaza. Halafu pia akawavulia adabu Maswahabah hata hivyo wakasimama upande wa al-Hajuuriy kwa batili. Wafuasi wake wakachukulia wepesi yale waliyosoma kuhusu kumuadhimisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake. Mwanzoni alikuwa anaonelea kuwa kuwapiga vita Raafidhwah ni fitina ambapo wakawa wamesimama upande wake. Baadaye akawa ameonelea kuwa ni Jihaad ambapo na wao wakawa wameonelea vivyo hivyo. Baadaye tena akanyamaza na kusimama juu ya hilo na wao wakawa wamefanya hali kadhalika. al-Hajuuriy amebadilisha mafundisho ya Dammaaj ambayo tulikuwa twayatambua. Pamoja na hayo yeye anasema kuwa Dammaaj haikubadilika na wafuasi wao wamekaa kimya.
Kwa ufupi ni kuwa al-Hajuuriy hatofautiana na mwanachuoni yeyote na hasemi wala hazungumzi neno isipokuwa msimamo wa wafuasi wake unajulikana. Wakati huo usiulizie msimamo wao kwa kuwa wao wamefungamana na al-Hajuuriy sawa awe juu ya haki au juu ya batili. Msimamo wao ni kusimama upande wa al-Hajuuriy na kuwa na ushabiki kwake. Wanachuoni wanaweza kupatia na kukosea. Inapokuja kwa al-Hajuuriy hakuna anachosema isipokuwa ni haki tupu!
- Mhusika: Shaykh Abu ´Ammaar ´Aliy al-Hudhayfiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://m-noor.com/showthread.php?p=33728
- Imechapishwa: 22/01/2017

[1] Tazama 156
[2] Tazama 887
[3] Tazama 1234
Mhusika: Shaykh Abu ´Ammaar ´Aliy al-Hudhayfiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://m-noor.com/showthread.php?p=33728
Imechapishwa: 22/01/2017
https://firqatunnajia.com/kasumba-ushabiki-vituko-na-vitakuro-vya-hajaawirah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)