Swali: Mawalii wa Allaah wanakuwa na karama baada ya kufa kwao?

Jibu: Baada ya kufa kwao zinaisha. Karama tena zitatoka wapi? Kutoka kwa maiti? Zinaisha. Matendo yake yamekatika na ametoka katika dunia hii na amebaki hana kitu isipokuwa matendo yake aliyotenda kabla ya kufa au zile du´aa au msamaha anaoombewa na nduguze waislamu au swadaqah. Haya ndio yaliyobaki na ndio yatayomwandama.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (05) http://alfawzan.af.org.sa/node/2048
  • Imechapishwa: 19/11/2016