Swali: Siku hizi waandishi wa magazeti wamekuwa wakiwashambulia wanachuoni na wanafunzi. Ni upi msimamo wetu kuhusiana na hilo?

Jibu: Kukataza maovu haya, ima kwa kuzungumza na kuandika au kwa moyo ikiwa hamuwezi kuandika. Kemea maovu haya angalau kwa moyo wako.

Matusi haya yatawageukia wao karibuni – Allaah akitaka. Kwa kuwa mwenye kutaka kupambana na haki na kuizuia ni lazima atakuja kujuta huko mbeleni. Haki siku zote iko na Mwenye kuinusuru, Naye si mwingine ni Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala):

لِيُحِقَّ الْحَقَّ وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ

“Ili Athibitishe haki na abatilishe ubatilifu japokuwa watachukia wahalifu.” (08:08)

Watu hawa wanazidhuru nafsi zao wenyewe. Kila mmoja ataulizwa juu ya maneno yake:

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ

“Hatamki kauli yeyote ile isipokuwa yuko karibu naye mwangalizi amejitayarisha [kurekodi].” (50:18)

Kila mmoja ataulizwa juu ya yale aliyoyaandika kwa mkono wake. Wataulizwa siku ya Qiyaamah. Anajipelekea katika adhabu yenye kuja kwa haraka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-1-18.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020