Ahl-ul-Bid´ah wa leo ni khatari kuliko wa kale

Swali: Katika maneno ya Salaf kumekuja matahadharisho dhidi ya Ahl-ul-Bid´ah. Je, waliyosema Salaf kuhusu watu wa Bid´ah yanaendelea mpaka siku ya Qiyaamah?

Jibu: Zama za mwisho yatazidi. Haya yatazidi katika zama za mwisho. Wakati ujinga na upotevu vitakuwa vingi watakuwa wanawachukia Salaf na kuwasema vibaya zaidi kuliko wale wa mwanzoni. Watu wa mwanazoni walikuwa na elimu hata kama walikuwa na upotevu. Lakini hawa wa leo, si elimu hawana wala taqwa hawana. Isitoshe wanawatukana Salaf na kuwafanyia maskhara. Mambo leo yamekuwa ni khatari na tunaomba kinga kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-1-18.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020