Kafara kwa kujiharamishia kitu cha halali

Swali: Ni ipi hukumu endapo mwanamke atajiharamishia kufanya kitu fulani? Je, analazimika kutoa kafara?

Jibu: Ndio. Ikiwa ameharamisha kitu halali basi anatakiwa kutoa kafara. Atatoa kafara ya kiapo. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ

“Ee Nabii! Kwanini unaharamisha kile alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu. Allaah amekwishakufaridhishieni ukomboaji kwa viapo vyenu.”[1]

[1] 66:01-02

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/110/%D9%85%D8%A7%D8%B0%D8%A7-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D9%85%D9%86-%D9%82%D8%A7%D9%84–%D8%B9%D9%84%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%B1%D8%A7%D9%85-%D9%85%D8%A7-%D8%A3%D9%81%D8%B9%D9%84-%D9%83%D8%B0%D8%A7-
  • Imechapishwa: 24/11/2019