Jirani hataki suluhu na mwenzake

Swali: Kuna mtu amefahamiana vibaya na jirani yake na wakakasirikiana. Mmoja wao anamtolea salamu mwenzake lakini huyo anayetolewa hamuitikii salamu. Je, wote wawili ni wenye kupata dhambi?

Jibu: Hapana, yule mwenye kutoa salamu ametekeleza wajibu wake. Mwenye kupata dhambi ni yule asiyeitikia salamu na ameacha jambo la wajibu juu yake na hataki suluhu. Huyu ndiye mwenye kupata dhambi. Ama yule anayetoa salamu, ametekeleza wajibu wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (68) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-05-21.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020