Swali: Je, kafara ya usengenyi ni du´aa?

Jibu: Usengenyi ni katika kuwadhulumu watu. Ikiwa wale aliowadhulumu watamsamehe na kumsamehe kosa hilo au yeye akawaombea du´aa na kuwataja kwa maneno mazuri anayoyajua kuhusu wao na vilevile akatubia kwa Allaah na kujutia alilofanya na akafidia kwa kuwataja kwa sifa njema badala ya zile mbaya alizozitaja, basi inatarajiwa Allaah atamsamehe.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31155/ما-هي-كفارة-الوقوع-في-الغيبة
  • Imechapishwa: 09/10/2025