Swali: Kijana huyu anasema, naeshi peke yangu na baba yangu ameoa mwanamke ambaye sio mama yangu. Mke wake amemlazimisha kuweka dishi/king´amuzi nyumbani kwake. Nimemnasihi mara nyingi lakini amekataa na wala hajali yale ninayomwambia mpaka amefikia kunifukuza nyumbani. Nifanye nini?
Jibu: Wewe umetekeleza wajibu wako pale ambapo umemnasihi na ukambainishia na hakukubali, wewe umetekeleza wajibu wako. Lakini ikiwa uko nyumbani, usikae wakati wanapotazama chaneli hizi. Usikae. Nenda kwenye chumba kingine au mahala pengine. Na ikiwa unaweza kuhama kutoka nyumbani na kueshi peke yako, itakuwa ni lazima kwako kufanya hivi kujiweka mbali na makazi ya shari. Ikiwa huwezi kuhama kwenye nyumba yako mwenyewe na huwezi kujenga nyumba kwa mali yako, baki kwenye nyumba ya baba yako lakini uwe kwenye chumba mbali na shari [hii wanayotazama]. Ama ikiwa unaweza kuhama na kueshi nje ya baba yako, itakuwa ni lazima kwako kufanya hivi.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/5426
- Imechapishwa: 28/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)