Jino moja kubwa sawa na mlima wa Uhud

Swali: Hadiyth inasema:

“Hakika siku ya Qiyaamah ataletwa mtu mkubwa na mnene na hatokuwa na uzito mbele ya Allaah sawa na ubawa wa mbu.”[1]

Je, hapa tunapata faida kwamba watafufuliwa siku ya Qiyaamah wakiwa na uzito na urefu wao?

Jibu: Inategemea kwa baadhi ya watu katika jambo hili inapokuja kwa makafiri. Kuhusu watu wa Peponi watakuwa na umri sawa na urefu wa dhiraa sitini. Kuhusu watu wa Motoni wanatofautiana; baadhi yao jino moja tu ni kama mlima wa Uhud. Hilo ni jino tu. Watafanywa wakubwa ndani ya Moto.

[1] al-Bukhaariy (4729) na Muslim (2785).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24477/كيف-تكون-اعمار-واطوال-الناس-يوم-القيامة
  • Imechapishwa: 18/10/2024