Jini linamtisha juu ya kujitibu kwa Qur-aan na nyuradi

Swali: Ninatatizwa na jambo ambalo nachelea lisije kunifikisha katika shirki, nalo ni kwamba kuna jini ninaliogopa. Nimejaribu kujitibu kwa kusoma Qur-aan na kumtegemea Allaah lakini pasi na mafanikio yoyote. Ni ipi dawa?

Jibu: Usikate tamaa hata siku moja.  Endelea kusoma Qur-aan na omba kinga dhidi ya shaytwaan. Usikate tamaa hata siku moja. Allaah (Jalla wa´Alaa) amesema:

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۚ إِنَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

“Na pindi utakapokuchochea uchochezi kutokana na shaytwaan, basi taka ulinzi kwa Allaah. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa kila kitu.” (07:200)

Soma nyuradi za asubuhi na jioni, soma Aayat Kursiy, al-Ikhlaasw, an-Naas na al-Kaafiruun. Hii itakuwa ni kinga kwako dhidi ya shaytwaan kwa idhini ya Allaah (´Azza wa Jall). Usikate tamaa kabisa. Shaytwaan asikukatishe tamaa ya nyuradi na kusoma Qur-aan. Kwa sababu atakukatisha tamaa na kukutia wasiwasi. Lakini hata hivyo usivunjike moyo hata siku moja. Dumu kwa kusoma nyuradi asubuhi na jioni na ukithirishe kumdhukuru Allaah na kuomba kinga dhidi ya shaytwaan aliyetiwa mbali na rahmah za Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15201
  • Imechapishwa: 28/06/2020