Swali: Jini anaweza kumuingia jini na akamuathiri mwenendo wake na akazungumza kupitia ulimi wake wakati anaposomewa Qur-aan?

Jibu: Bila ya shaka, linatokea hili. Bila ya shaka jini humgusa mtu na kupita kwenye mwili wake kama damu inavopita kwenye mishipa ya damu. Linamgusa pia:

كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ

“… kama anavyosimama yule aliyezugwa na shaytwaan kwa kuguswa.” (02:275)

Ukweli wa mambo unatolewa ushahidi na hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-02-09.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014