Wanachuoni wamesema kuwa ni wajibu kwa waislamu kufanya Jihaad angalau mara moja kwa mwaka. Wawapige Jihaad maadui wa Allaah. Lengo ni ili neno la Allaah liweze kuwa juu. Lengo sio kwa sababu ya kutetea nchi kwa dhati yake. Kutetea nchi kwa dhati yake ni jambo lililo kwa muumini na kafiri. Hata makafiri wanatetea nchi zao. Lakini muumini anaitetea dini ya Allaah. Anatetea nchi lakini hata hivyo sio kwa dhati yake. Anatetea nchi yake kwa sababu ni nchi ya Kiislamu. Hivyo anaitetea kwa ajili ya kuuhami Uislamu ambao ni suluhu katika nchi hii.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/34)
  • Imechapishwa: 17/01/2023