Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

55 – Kama ilivyotajwa na Kitabu cha Mola wetu:

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ

“Kuna nyuso siku hiyo zitanawiri. Zikimtazama Mola wake.”[1]

56 – Tafsiri yake ni kama alivokusudia Allaah (Ta´ala) na kujua.

MAELEZO

Aayah hii inasema wazi kwamba Allaah ataonekana kwa macho, kwa sababu kumetajwa kihusishi (إِلَى). Maana yake ni kuwa macho ndio yataona. Mu´tazilah wanasema kuwa (إِلَى) ni wingi wa neema. Kwa maana nyingine wataona neema za Mola wake. Makengeusho haya yanachekesha kwa sababu viambishi havina wingi. Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tafsiri yake ni kama alivokusudia Allaah (Ta´ala) na kujua.”

Bi maana inatakiwa kufahamika kama alivyotaka Allaah, nako ni kuonekana kwa macho na si kama walivyofasiri wazushi.

[1] 75:22-23

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 17/01/2023