Swali: Vipi kumraddi yule mwenye kusema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuitikia jibu la mjakazi na badala yake alitabasamu tu kwa sababu alikuwa bado ni mdogo?

Jibu: Alisema kuwa ni muumini:

“Mwache huru. Kwani kwa hakika ni muumini.”

Ni nani aliyesema kuwa alitabasamu kwa kuwa alikuwa bado ni mdogo? Ni nani aliyesema kuwa alikuwa mdogo? Mtoto mdogo huulizwa? Ni mtu mkubwa ambaye anaelewa swali. Watu hawa wanatilia ukaidi usiokuwa na maana. Malengo yao ni kufuta dalili na kunusuru kauli ya Mu´attwilah. Haya ndio malengo yao. Baadhi yao wanafikia mpaka kusema ya kwamba Hadiyth isemayo “Allaah Yuko wapi?” maana yake ni “Allaah ni nani?” Bi maana “Wapi” maana yake ni “Nani”. Je, “Wapi” katika lugha ya kiarabu maana yake ni “Nani”? Watu hawa wanajibebetua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340324.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2015