Je, ni wajibu kwa aliyechinja kabla ya swalah kumchinja mnyama mwingine badala yake baada ya swalah?

Swali: Wale wenye kuona kuwa ni wajibu kuchinja Udhhiyah wakijengea hoja kwa kitendo hichi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha ambaye amechinja kabla ya swalah kumchinja mnyama mwingine badala yake baada ya kumalizika kuswali na wakasema kuwa hiyo inafahamisha kuwa ni wajibu.

Jibu: Dalili zingine zimefahamisha kuwa inapendeza, ikiwa ni pamoja na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Utapoingia mwezi wa Dhul-Hijjah na akataka mmoja wenu kuchinja, basi asikate kutoka katika nywele wala kucha zake chochote mpaka achinje kwanza.”[1]

[1] Muslim.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24021/ماذا-يجب-على-من-ضحى-قبل-الصلاة
  • Imechapishwa: 17/08/2024