66. Utangulizi ambao wanafunzi wanatakiwa kuuhifadhi

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Nimetanguliza utangulizi huu kwa sababu ambaye ataelewa utangulizi huu basi atajua uongofu uko wapi katika mada hii na nyenginezo.

MAELEZO

Msingi wa kitabu hiki ni kujibu yale yanayosemwa na wanazuoni juu ya majina na sifa za Allaah. Kabla ya kumjibu muulizaji, ametanguliza dibaji hii unaoitwa ”utangulizi wa al-Hamawiyyah”. Ni utangulizi mtukufu ambao wanafunzi walikuwa wakiuwekea umuhimu na kuuhifadhi. Kwa sababu ndani yake kuna kanuni za wazi mwanafunzi anafaidika nazo na anapambanua kati ya elimu ya Salaf na elimu ya wale waliokuja nyuma. Njia ya uongofu ni ile iliyopitwa juu yake na Salaf, na kwamba njia ya upotofu ni ile iliyopitwa juu yake na wengi katika wale waliokuja nyuma.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 104
  • Imechapishwa: 18/08/2024