Swali: Ni sababu gani Salaf (Rahimahumu Allaah) walikuwa na msimamo mkali katika baadhi ya masuala ya ´Aqiydah? Kwa mfano suala la Allaah kuwa juu na Allaah kuonekana Aakhirah na kwamba Qur-aan ni maneno ya Allaah (´Azza wa Jall) na hayakuumbwa?

Jibu: Hawakuwa na msimamo mkali. Walifuata aliyoteremsha Allaah na wakayaamini na kumraddi mwenye kupinga hilo na kuziharibu Aayah za Allaah. Kufanya hivi hakuitwi kuwa ni kuwa na msimamo mkali. Kunaitwa “kushikamana bara barana kuamini aliyoteremsha Allaah”. Tupeni amani na kusema kuwa tuna msimamo mkali! Badala yake sema “kushikamana barabara na aliyoteremsha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-6-8.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020