Je, Mtume anaonyeshwa matendo ya Ummah wake?

Swali: Nimesikia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya kaburi lake tukufu anayajua matendo ya watu hii leo. Je, maneno haya ni kweli au si kweli? Je, wakati muislamu anaposema:

السلام عليك أيها النبي ورحمة الله وبركاته

“Amani iwe juu yako, ee Nabii, na rehema na baraka za Allaah.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasikia salamu na kumwitikia? Je, ni kweli?

Jibu: Kuhusu kumtolea salamu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka kwa Ummah wake anaonyeshwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na anafikishiwa popote anapokuwa pindi tunapomtolea salamu popote tulipo ulimwenguni. Kuhusu matendo ya Ummah wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sijui kama ni kweli au si kweli.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (07) http://binothaimeen.net/content/13574
  • Imechapishwa: 07/11/2020