Je, mbwa wanaoruhusiwa katika Shari´ah wanawazuia Malaika kuingia ndani ya nyumba?

Swali: Je, Malaika kujizuia kuingia nyumba yenye mbwa kunajumuisha mbwa wa mawindo?

Jibu: Hapana, hakujumuishi. Makusudio ni yule mbwa ambaye hakuidhinishwa, kama ilivyotangulia katika somo lililotangulia. Mbwa na picha zilizoidhinishwa hazizuilii. Picha zenye kudhalilishwa hazizuii kuingia kwa Malaika. Ndio maana Jibriyl alimwambia:

“Ifanye mito miwili.”[1]

Hapo ndipo Jibriyl aliingia ndani baada ya kuifanya pazia na mto. Vivyo hivyo mbwa ambaye hakuruhusiwa ndiye ambaye anawazuia. Kuhusu picha walioruhusiwa kama vile mbwa wa mawindo, mbwa wa kuelekeza njia na mbwa kwa ajili ya ulinzi hawawazuilii.

[1] at-Tirmidhiy (2806) na Abu Daawuud (4158).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24127/هل-يمنع-كلب-الصيد-دخول-الملاىكة-للبيت
  • Imechapishwa: 06/09/2024