Swali: Nawasomea wagonjwa wa akili na neva kama vile kwa kuwasomea al-Faatihah, Aayah al-Kursiy, al-Falaqa na an-Naas na du´aa zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nawasomea yale yaliyotajwa ndani ya Qur-aan Tukufu kama mfano wa asali na mafuta ya zeituni na kuwaambia wagonjwa wavitumie katika chakula na kujipaka. Kwa idhini ya Allaah nimewaponesha watu wengi. Bado naendelea kufanya hivo na hakuna yeyote niliyemwomba malipo. Je, kitendo changu kinafaa?
Jibu: Mgonjwa anatakiwa kutibiwa kwa kusomewa Qur-aan, Sunnah na du´aa zilizowekwa katika Shari´ah pamoja na asali, haba soda na mfano wake. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ
“Tunateremsha katika Qur-aan ambayo ni shifaa na rehema kwa waumini.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia yule Swahabah ambaye alimfanyia matabano yule bwana ambaye aliumwa na nyoka ambapo akamsoma al-Faatihah na akapona:
“Umejuaje kuwa [Suurah hii] ni matabano?”[2]
Allaahu (Ta´ala) amesema:
يَخْرُجُ مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِّلنَّاسِ
“Kinatoka katika matumbo yao kinywaji cha rangi mbalimbali – ndani yake mna shifaa [ya magonjwa] kwa watu.”[3]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu haba soda:
“Ni ponyo ya kila ugonjwa isipokuwa tu mauti.”[4]
Muda wa kuwa unatibu kwa namna hiyo, basi aendelea kufanya hivo.
[1] 17:82
[2] al-Bukhaariy (2276) na Muslim (2201).
[3] 16:69
[4] al-Bukhaariy (5687) na Muslim (2215).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/13-14)F
- Imechapishwa: 29/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/13-14)F
Imechapishwa: 29/07/2026
https://firqatunnajia.com/je-matabano-haya-yanafaa/