Swali: Je, muislamu pindi atakapoingia Peponi atawatambua ndugu zake walioko Peponi? Je, ataikumbuka familia yake baada ya kufa kwake na kujua hali zao?
Jibu: Ndio, atawakumbuka jamaa zake na wengineo waliokuwa wakimfurahisha. Allaah (Ta´ala) amesema:
يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ ۖ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ ۖ وَأَنتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
“Watapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe na humo mna yale zinazotamani nafsi na ya kuburudisha macho nanyi humo ni wenye kudumu.”[1]
Bali ni kwamba mtu ataishi na familia yake katika ngazi moja. Hapo ni pale ambapo baadhi ya wanafamilia wako katika ngazi za chini kuliko wengine. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَا أَلَتْنَاهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَيْءٍ ۚ كُلُّ امْرِئٍ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ
“Wale walioamini na dhuriya yao ikawafuata kwa imani Tutawakutanisha nao dhuriya yao na hatutawapunguzia katika matendo yao chochote. Kila mmoja ni mwenye jukumu juu ya matendo yake.”[2]
Hata hivyo mimi sijui mapokezi sahihi juu ya kwamba maiti atajua hali ya familia yake ulimwenguni. Lakini baadhi ya matukio yanajulisha kuwa mtu anaweza kujua baadhi ya mambo yanayoendelea ulimwenguni. Kuna mtu alinieleza kuwa baada ya baba yake kufa alipoteza hati yake, ambapo baada ya hapo akamuota baba baba yake akimweleza kuwa hati hiyo ilikuwa imekwama kwenye daftari la mtu mwingine. Hili linathibitisha kuwa mtu anaweza kuyajua mambo kadhaa yanayoendelea kwa familia yake – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] 43:71
[2] 52:21
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/450-451)
- Imechapishwa: 29/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/450-451)
Imechapishwa: 29/07/2026
https://firqatunnajia.com/385-je-maiti-anajua-yanayofanywa-na-familia-yake/