110 – Haipaswi kuwekea mipaka ya siku tatu kwa ajili ya kutoa pole, kiasi kwamba isiwezekane zaidi ya hapo, bali inapofikiriwa kuwa kuna manufaa katika kutoa pole basi afanye hivyo. Kwa sababu imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa alitoa pole baada ya kupita siku tatu, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth ya ´Abdullaah bin Ja´far (Radhiya Allaahu ´anhuma) aliyesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituma jeshi na akamfanya Zayd bin Haarithah kuwa kiongozi wao ambapo akasema: ”Iwapo Zayd atauawa au kuuliwa hali ya shahidi basi kiongozi wenu awe Ja´far, akiuawa au kuuliwa hali ya shahidi basi kiongozi wenu awe ´Abdullaah bin Rawaahah. Basi wakakutana na adui. Zayd akachukua bendera, akapigana mpaka akauawa, kisha Ja´far akachukua bendera, akapigana mpaka akauawa, kisha ´Abdullaah akachukua bendera, akapigana mpaka akauawa, kisha bendera ikachukuliwa na Khaalid bin al-Waliyd ambapo Allaah akamfungulia ushindi. Kisha khabari yao zikamfikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akatoka kwa watu, akamsifu Allaah na akamhimidi, kisha akasema: ”Ndugu zenu wamekutana na adui. Hakika Zayd alichukua bendera na akapigana mpaka akauawa na akauliwa hali ya kuwa shahidi, kisha… kisha… kisha bendera ikachukuliwa na upanga kati ya mapanga ya Allaah, kwa maana ya Khaalid bin al-Waliyd, basi Allaah akamfungulia ushindi. Kisha akachelewa kuwazuru watu wa nyumba ya Ja´far kwa muda wa siku tatu, kisha akawaendea ambapo akasema: “Msimlilie ndugu yangu baada ya leo, nileteeni watoto wa ndugu yangu” basi tukaletwa kana kwamba sisi ni vifaranga. Akasema: “Nileteeni kinyozi.” basi tukaletewe kinyozi ambapo akanyoa vichwa vyetu. Kisha akasema: “Ama Muhammad anafanana na mjomba wetu Abu Twaalib. Na ´Abdullaah anafanana nami kwa sura na tabia.” Kisha akanishika mkono wangu ambapo akauinua, akasema:
اللهم اخلف جعفرا في أهله، وبارك لعبد الله في صفقة يمينه، قالها ثلاث مرات
“Ee Allaah! Mpe Ja´far mrithi mwema kwa familia yake na mbariki ´Abdullaah katika biashara ya mkono wake wa kulia.” Alisema hivo mara tatu.”
Kisha mama yetu akaja na akamueleza kuhusu uyatima wetu na akaanza kumhurumia, basi akasema: “Je, unaogopa juu yao umasikini, hali ya kuwa mimi ni mlinzi wao katika dunia na Aakhirah?”
Ameipokea Ahmad (1750) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kwa mujibu wa masharti ya Muslim. Pia al-Haakim (3/298) amepokea sehemu yake kupitia njia yake. Abu Daawuud na an-Nasaa’iy wamepokea sehemu ya kisa cha kuchelewa kwa siku tatu pamoja na kunyoa nywele. Sehemu nyingine imeshatangulia katika masuala ya 18, uk. 21. al-Haakim amesema:
”Cheni ya wapokezi ni Swahiyh.”
na adh-Dhahabiy ameafikianan yake.
Hadiyth ina nyingine inayoitia nguvu katika “al-Musnad” (3/467), lakini ndani yake kuna unyonge.
Baadhi ya wanafunzi wa Imaam Ahmad wameona vile tulivyoona ya kwamba tanzia haina kikomo cha muda, kama ilivyokuja katika ”al-Inswaaf” (2/564), na hilo ni moja ya maoni ya madhehebu ya Shaafi´iy ambao wamesema:
”Kwa sababu lengo ni kufanya du´aa, kuwahamasisha watu kuwa na subira na kuwazuia na huzuni, jambo ambalo linaweza kufanyika hata baada ya muda mrefu.”
Amesimulia hayo Imaam al-Haramayn na akaliweka wazi Abul-´Abbaas bin Al-Qaasw ambaye ni mmoja wa maimamu wao. Hata kama baadhi yao walikataa maoni hayo, basi walifanya hivyo kwa kutegemea tu maoni maarufu katika madhehebu si kwa hoja ya Kishari´ah. Tazama: “al-Majmuu´” (5/306).
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 209-210
- Imechapishwa: 30/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 209-210
Imechapishwa: 30/07/2026
https://firqatunnajia.com/108-hakuna-mpaka-wa-tanzia/