Je, kuna dalili ya anayeingia katika Ihraam kuoga?

Swali: Je, kumethibiti dalili yoyote kuhusu kuoga isipokuwa kuamrishwa mwanamke mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi?

Jibu: Ndiyo, Hadiyth ya Zayd bin Thaabit:

“Alivua nguo zake kwa ajili ya kuingia ndani ya Ihraam na akaoga.”

Hadiyth ya Ibn ´Umar:

“Ni katika Sunnah kuoga.”

Hadiyth ya Jaabir inayosema:

Asmaa´ bint Umays alijifungua Muhammad bin Abiy Bakr akiwa katika Dhul-Hulayfah ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha akoge.”

Vivyo hivyo ´Aaishah alikuwa mwenye hedhi ambapo akamwamrisha aoge.

Ikiwa wanawake waliokuwa katika hedhi na damu ya hedhi waliamriwa kuoga ingawa hawahitajiki kuswali wala kujitwajihirisha, basi wasiokuwa wao wana haki zaidi ya kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24943/ما-دليل-استحباب-الغسل-للمحرم
  • Imechapishwa: 11/01/2025