Je, kila muislamu ni muumini na kinyume chake?

Swali: Je, mtu anaweza kuwa muislamu na tusimwite ´muumini`?

Jibu: Kuna makinzano baina ya Ahl-ul-Sunnah wal-Jamaa‘ah; kwa sababu muislamu ni mpana zaidi kuliko muumini, na muumini ni maalum zaidi. Kwa hivyo kunaposemwa ´muislamu´ kunakusanywa wote wawili: waislamu, waumini na wenye kufanya ihsaan. Lakini muislamu anaweza kutajwa na sifa ya Uislamu bila ya imani kamili wakati wa kudhihirisha hali ya sifa. Ikiwa ni miongoni mwa wenye kufanya maasi kunasemwa `muislamu´, katika hali hiyo si muumini wa imani kamili. Hata hivyo bora zaidi katika hali hii ni kusema ´muumini mwenye imani pungufu´, ´muumini fasiki´ au “muumini kwa imani yake na fasiki kwa dhambi yake kubwa´, kama alivyosema Abul-‘Abbaas [Ibn Taymiyyah] katika “al-‘Aqiydah al-Waasitwiyyah”, kwa sababu daraja la sifa ya imani ni kubwa sana. Allaah amepambanua kati ya hayo mawili pale aliposema:

إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ

“Hakika waislamu wanaume na wanawake na waumini wanaume na waumini wanawake… ”[1]

Hii ni katika muktadha wa kupambanua.

“Hazini mwenye kuzini pale anapozini hali ya kuwa ni muumini, hanywi pombe mwenye kunywa pombe pale anapokunywa hali ya kuwa ni muumini na wala hapori kitu, jambo linalofanya watu kumuinulia macho, hali ya kuwa ni muumini.”[2]

Ni muislamu. Kwa msemo mwingine si muumini mwenye imani kamili; ile imani anayostahili mwenye nayo kupewa sifa kamili. Hivyo basi ni lazima kuoanisha maandiko kwa namna inayoweza kuleta uwiano na kuweka wazi maana yake.

[1] 33:35

[2] Hadiyth ni Swahiyh na cheni ya wapokezi wake ni nzuri. Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengineo kupitia njia nyingine kutoka kwa Abu Hurayrah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25084/هل-كل-مسلم-مومن-او-العكس
  • Imechapishwa: 09/02/2025