Swali: Kipi kinachompasa mjinga anayeabudia kaburi?

Jibu: Hii ni miongoni mwa mambo makubwa ambayo yameletwa na Uislamu na Mitume. Haifichiki kwa yeyote, kwani Qur-aani iko mikononi mwao, Sunna iko mikononi mwao na wanazuoni wako mikononi mwao. Lakini wao wamekinai na kile walichonacho, hawataki kuonywa. Tunamuomba Allaah atuepushe na hili.

Isitoshe kama itakadiriwa kuwa ni wajinga, basi hukumu ya duniani kwa hili ni kama ya makafiri wengine. Lakini kuhusu Aakhirah, ikiwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anajua katika nyoyo zao kwamba ni wajinga na wanatafuta haki, basi watakuwa na hukumu ya Aakhirah mbele ya Allaah. Allaah atasimamia hesabu yao, kama Ahl-ul-Fatrah. Wanaweza kujaribiwa siku ya Qiyaamah. Allaah amebainisha kuwa wengi wao hawatii akilini wala hawafahamu. Amesema (Ta´ala):

إِنَّهُمُ اتَّخَذُوا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ

”Hakika wao wamewafanya mashaytwaan kuwa marafiki badala ya Allaah na wanafikiri kuwa wao wameongoka.”[1]

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُمْ بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا

“Sema: “Je, Tukujulisheni ni wepi ambao matendo yao yamekhasirika? Ni wale ambao wamepoteza juhudi zao katika uhai wa dunia nao wakidhani kwamba wanatenda vizuri.”[2]

[1] 07:30

[2] 18:103-104

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25087/ما-حكم-القبوري-الجاهل
  • Imechapishwa: 09/02/2025