Swali: Je, kisa cha kunyonyeshwa kwa Saalim mtumwa huru wa Abu Hudhayfah ni maalum kwake tu au kinamuhusu pia mwenye hali kama ya Saalim? Je, inajuzu kunyonyesha mtu mzima ikiwa kutahitajika?
Jibu: Sahihi ni kwamba haijuzu kunyonyesha mtu mzima. Hili lilikuwa maalum kwa Saalim au limefutwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakuna kunyonyesha isipokuwa ndani ya miaka miwili.”
Hakuna kunyonyesha isipokuwa kabla ya kuachishwa ziwa. Hakika kunyonyesha ni kwa ajili ya njaa. Haya ndio maoni sahihi ambayo jopo kubwa la wanazuoni wanaonelea hivo.
Kisa cha Saalim ima kimefutwa, kama walivyosema kikosi kikubwa cha wanazuoni, au kilikuwa maalum kwake, kama walivyosema wengine. Wake wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – akiwemo Umm Salamah – amesema:
”Tulikuwa tukiona hili ni jambo maalum kwa Saalim, isipokuwa tu ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30955/هل-يجوز-ارضاع-الكبير-اذا-دعت-الحاجة
- Imechapishwa: 18/09/2025
Swali: Je, kisa cha kunyonyeshwa kwa Saalim mtumwa huru wa Abu Hudhayfah ni maalum kwake tu au kinamuhusu pia mwenye hali kama ya Saalim? Je, inajuzu kunyonyesha mtu mzima ikiwa kutahitajika?
Jibu: Sahihi ni kwamba haijuzu kunyonyesha mtu mzima. Hili lilikuwa maalum kwa Saalim au limefutwa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakuna kunyonyesha isipokuwa ndani ya miaka miwili.”
Hakuna kunyonyesha isipokuwa kabla ya kuachishwa ziwa. Hakika kunyonyesha ni kwa ajili ya njaa. Haya ndio maoni sahihi ambayo jopo kubwa la wanazuoni wanaonelea hivo.
Kisa cha Saalim ima kimefutwa, kama walivyosema kikosi kikubwa cha wanazuoni, au kilikuwa maalum kwake, kama walivyosema wengine. Wake wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – akiwemo Umm Salamah – amesema:
”Tulikuwa tukiona hili ni jambo maalum kwa Saalim, isipokuwa tu ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).”
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30955/هل-يجوز-ارضاع-الكبير-اذا-دعت-الحاجة
Imechapishwa: 18/09/2025
https://firqatunnajia.com/je-inajuzu-kumnyonyesha-mtu-mzima-haja-ikipelekea-kufanya-hivo/