Je, inafaa kwa mwanamke kurejea kwa hiba ya mumewe?

Swali: Kurejea kwa mwanamke katika hiba yake kwa mumewe?

Jibu: Ikiwa ana sababu, kama vile kumpa zawadi kwa kukhofia talaka kisha akamtaliki, ana haki ya kurejea. Lakini ikiwa alimpa kwa sababu ya umasikini wake na uhitaji, si kwa khofu ya talaka, basi hana haki ya kurejea, kwani inajumuishwa na Hadiyth. Kinachokusudiwa ni kwamba inapaswa kuzingatiwa dalili na mtu amche Allaah. Ikiwa dalili zinaonyesha kuwa nwanamke alimpa zawadi kwa kukhofia shari yake, kwa kukhofia asimwache au kwa kukhofia mwanaume asioe mke mwingine, kisha akafanya kinyume na matarajio yake, basi amrudishie mwanamke zawadi yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25382/هل-للمراة-الرجوع-في-هبتها-لزوجها
  • Imechapishwa: 08/03/2025