Je, ´ibaadah ni zenye kumuwajibikia mtu mwenye ugonjwa wa neva?

Swali: Kwa mujibu wa maneno ya madaktari mgonjwa anaumwa wa neva wa muda mrefu. Ugonjwa huu ulimletea matatizo mengi ikiwa ni pamoja na kuwanyuanyulia sauti mahuzuniko, kuwakata ndugu na kupatwa na wasiwasi, aibu na khofu. Je, kunamdondoka yale mambo ya wajibu wa ki-Shari´ah?

Jibu: Yale mambo ya wajibu wa ki-Shari´ah hayamdondoki midhali bado yuko na akili. Lakini pale ambapo akili yake itamwondoka na akashindwa kuidhibiti akili yake, basi hapo ndio atakuwa mwenye kupewa udhuru. Kile ninachomnasihi ni kwamba aombe du´aa, kumtaja Allaah (´Azza wa Jall) na kumwomba msamaha kwa wingi. Namshauri pia kumwomba Allaah msaada dhidi ya shaytwaan pale inapoanza hasira yake. Pengine kwa kufanya hivo akamponya.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/465)
  • Imechapishwa: 20/07/2026