379. Kuzikwa karibu na mtoto kunamwondoshea adhabu maiti?

Swali: Baadhi ya watu ambao wanafisha ndugu wanapupia kumzika karibu na mtoto na wanamjengea dhana nzuri kwa hilo na kwamba kitendo hicho kina sifa ya kipekee. Ni ipi hukumu ya jambo hili?

Jibu: Kitendo hichi hakina msingi. Mtu ndani ya kaburi lake ima anaadhibiwa au kustareheshwa kutokana na matendo yake, na si kutokana na ambaye ni jirani yake. Kwa ajili hiyo hakuna msingi wa kitendo hichi kabisa. Ukweli wa mambo ni kwamba maiti ndani ya kaburi lake ima anaadhibiwa au kustareheshwa kutokana na matendo yake, ni mamoja majirani zake ni wema au waovu.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/444)
  • Imechapishwa: 20/07/2026